• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chereko za ubingwa zarindima Yanga, baada ya kuifunga Toto Afrika

    (GMT+08:00) 2017-05-17 08:45:10
    Shamrashamra za ubingwa zimeanza kurindima mitaa ya Jangwani, baada ya Yanga SC kuwachapa 'watoto wao', Toto Africans 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya jana uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

    Ushindi huo uliotokana na bao pekee la mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Amissi Joselyn Tambwe unaifanya Yanga ifikishe pointi 68 baada ya kucheza mechi 29 na itahitaji sare tu kwenye mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mbao FC kujihakikishia taji la ubingwa.

    Lakini hata sasa, Yanga wanaweza kuanza kushangilia ubingwa kutokana na hazina kubwa ya mabao waliyonao, kwani sasa Simba watatakiwa kuifunga Mwadui FC mabao 13-0 ili kuizuia timu ya Jangwani kutwaa taji kwa mara ya tatu la mfululizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako