• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa kamati ya Umoja wa Afrika atoa wito wa ushirikiano zaidi na Ulaya

    (GMT+08:00) 2017-05-17 09:12:40

    Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Mahamat ametoa wito wa kuwepo kwa ushirikiano wa karibu zaidi kati ya Afrika na Ulaya, ili kukabiliana na mabadiliko na changamoto zinazoikabili dunia. Bw. Mahamat alisema hayo jana alipohutubia bunge la Ulaya huko Strasbourg. Amesema mazingira ya kimataifa yanakabiliwa na mabadiliko ya kasi, ambapo nchi zinazojitokeza zinatafuta hadhi yao katika dunia ambayo imekuwa na ncha nyingi. Amesisitiza kuwa matumaini ya pekee ya kupata ufumbuzi wa kudumu, yanategemea juhudi za pamoja kwenye msingi wa mshikamano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako