• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Duru ya sita ya Mazungumzo ya amani ya Syria yaanza Geneva

  (GMT+08:00) 2017-05-17 09:57:45

  Duru ya sita ya mazungumzo ya amani kuhusu suala la Syria yanayoongozwa na Umoja wa Mataifa imeanza rasmi mjini Geneva.

  Mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia suala la Syria Bw Staffan de Mistura, amefanya mazungumzo na wajumbe wa pande zote, lakini hakutaja ni mambo gani yalizungumzwa.

  Ujumbe wa serikali ya Syria na makundi makubwa ya upinzani, na wawakilishi wa Misri na Russia pia walihudhuria mazungumzo hayo.

  Awali Bw Staffan de Mistura alisema mazungumzo ya duru hiyo yatakuwa mafupi na yenye ufanisi, na yatafuatilia mambo makuu manne, ikiwa ni pamoja na kuunda serikali ya maafikiano ya kitaifa, marekebisho ya katiba, kufanya uchaguzi mkuu na kapambana na ugaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako