• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa dola milioni 1 kuwasaidia wakimbizi wa ndani Somalia

    (GMT+08:00) 2017-05-17 10:05:30

    China imesaini makubaliano na Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM kuhusu kutoa msaada wa dola milioni 1 za kimarekani unaolenga kuunga mkono juhudi za Shirika hilo kuwasaidia wakimbizi wa ndani, jamii zilizo kwenye hatari na waliorudi kutoka ukimbizini nchini Somalia.

    Shirika hilo limetoa taarifa ikisema, mradi huo utakaowasaidia watu wapatao elfu 15, utaunga mkono Mpango wa Kibinadamu wa Somalia kwa mwaka huu, unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa na serikali ya nchi hiyo.

    Pia mradi huo utatoa msaada kwa wakazi wa maeneo yenye ukame nchini Somalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako