• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Nigeria zafanya mazungumzo kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kilimo

    (GMT+08:00) 2017-05-17 10:06:13

    China na Nigeria zimefanya mazungumzo ya kimkakati huko Abuja ili kuimarisha ushirikiano kati yao kwenye sekta ya kilimo.

    Mkutano huo wa Baraza la ushirikiano kwenye sekta ya kilimo kati ya China na Nigeria, umejadili jinsi China inavyoweza kuisaidia Nigeria katika masuala ya uzalishaji wa kilimo, usalama wa chakula na upunguzaji umaskini kwa lengo la kutimiza ukuaji endelevu wa uchumi.

    Balozi wa China nchini Nigeria Bw. Zhou Pingjian amesema, China ikiwa mwenzi wa kimkakati wa Nigeria, iko tayari kutoa uzoefu katika maendeleo ya kilimo na kutoa uungaji mkono wa kifedha na kiufundi katika kutimiza mipango ya nchi hiyo ya kukuza kilimo na kuimarisha usalama wa chakula.

    Pia amesema, China inapenda kushirikiana na Nigeria katika kuweka jukwaa lenye ufanisi zaidi ili kuvutia zaidi uwekezaji kutoka China katika sekta ya kilimo nchini Nigeria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako