• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaongeza usimamizi wa mtandao wa internet kufuatia kutokea kwa kirusi kibaya cha computer

    (GMT+08:00) 2017-05-17 18:53:35

    Serikali ya Kenya imewaondoa wasiwasi wananchi wake kuwa mfumo wa computer wa idara za serikali na mitandao yake viko salama kufuatia kutokea kwa kirusi cha computer kinachoenea kwa kasi na kuleta athari kubwa kwa watumiaji duniani.

    Waziri wa habari na teknolojia ya mawasiliano nchini Kenya Joe Mucheru amesema serikali inafuatilia kwa makini kirusi hicho ambacho kimeharibu zaidi ya computer laki mbili zinazotumia mfumo wa Windows katika nchi zaidi ya 150.

    Amesema serikali imeongeza usimamizi na ufuatiliaji wa mfumo huo ili kuzuia na kuondoa uwezekano wowote wa kutokea shambulizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako