• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uteuzi wa wagombea urais nchini Rwanda kufanyika mwezi Juni

  (GMT+08:00) 2017-05-17 18:54:18

  Tume ya Uchaguzi ya Rwanda (NEC) imeweka mwezi Juni kuwa mwisho wa kupokea fomu za kuomba kugombea nafasi ya urais, kabla ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Agosti.

  Katibu wa Tume hiyo Charles Munyaneza amesema, tarehe za mwisho za kupokea fomu za maombi ni kuanzia Juni 12 hadi 23. Amesema awamu ya pili ya kuhakiki vitabu vya wapiga kura imeanza na itaendelea mpaka mwisho wa mwisho huu. Ametoa wito kwa watu wote waliojiandikisha kushirikiana na maofisa wa maeneo husika kuhakiki taarifa zao kama ziko sahihi kwenye vitabu hivyo.

  Rwanda itafanya uchaguzi wa rais Agosti 4 mwaka huu, ukiwa ni uchaguzi wa tatu tangu kumalizika kwa utawala wa uliokuwepo baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako