• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kuanzisha kituo cha mkusanyiko wa takwimu Big Data cha taifa

  (GMT+08:00) 2017-05-17 20:41:20

  Tarehe 17 Mei ni Siku ya mawasiliano ya simu na jamii ya upashanaji wa habari ya mwaka 2017. Katika maadhimisho ya siku hiyo, China imesema itaanzisha kituo cha mkusanyiko wa takwimu Big Data cha taifa ili kuhimiza upashanaji wa habari kati ya idara mbalimbali na sehemu mbalimbali.

  Hayo yamesemwa na mhandisi mkuu wa Wizara ya viwanda na upashanaji wa habari IT ya China Bw. Zhang Fenga katika mkutano wa "Siku ya mawasiliano ya simu na jamii ya upashanaji wa habari ya mwaka 2017" uliofanyika leo mjini Beijing. Amesema kituo hicho pia kitaongeza ufanisi wa matumizi ya takwimu, kuimarisha usimamizi wa usalama, ili kupambana vikali na vitendo vya udukuzi na kuuza takwimu zinazohusu watu binafsi, na kulinda usalama wa takwimu kwenye mtandao wa Internet.

  Kauli mbiu ya mkutano huo kwa mwaka huu ni "kuendeleza mkusanyiko wa takwimu Big Data na kuongeza uwezo wa ushawishi".

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako