• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China na Tanzania zasaini makubaliano ya Tanzania kuingiza bidhaa za muhogo nchini China

  (GMT+08:00) 2017-05-17 21:06:10

  Serikali za China na Tanzania zimesaini makubaliano yanayoruhusu bidhaa za muhogo kuingia kwenye soko la China bila kutozwa ushuru, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na serikali ya China kuruhusu sehemu kubwa ya bidhaa za kilimo kutoka nchi za Afrika kuingia kwenye soko la China bila ushuru.

  Makubaliano hayo yalisainiwa jana hapa Beijing kati ya balozi wa Tanzania nchini China Mh Mbelwa Kairuki, na naibu mkuu wa idara ya usimamizi wa ubora, ukaguzi na karantini ya China Bw Li Yuanping, na kushuhudiwa na Waziri wa ujenzi, mawasiliano na uchukuzi wa Tanzania, Profesa Makame Mbarawa aliyemwakilisha Rais John Mgaufuli wa Tanzania kwenye mkutano wa ukanda mmoja, njia moja. Kusainiwa kwa makubaliano hayo, kuna maana Tanzania imekidhi vigezo vyote vya karantini vilivyowekwa na serikali ya China kuhusiana na uuzaji wa bidhaa za muhogo kwenye soko la China.

  Licha ya China kuwa na orodha kubwa ya bidhaa kutoka Afrika zinaweza kuingia kwenye soko lake bila ushuru, Utaratibu wa karantini wa China ni mkali na mchakato wake ni mrefu. Hii ni kutokana na hofu kuwa bidhaa zinazoingia kwenye soko la China kutoka kwenye nchi za kitropiki, kama hazikusimamiwa na kukaguliwa ipasavyo, zinaweza kuleta hatari ya kuingiza vijidudu na magonjwa ya mimea.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako