• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya yadhamiria kupambana na wanaoeneza chuki kabla ya uchaguzi mkuu

  (GMT+08:00) 2017-05-18 09:16:04

  Idara za usalama nchini Kenya ziko katika hali ya tahadhari ili kuwakamata na kuwashitaki watu wanaojihusisha na utoaji wa hotuba zinazochochea chuki katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu.

  Waziri wa mambo ya ndani Bw Joseph Nkaissery amesema serikali itapambana na wagombea wanaochochea jamii kubeba silaha, wakati kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu zikipamba moto. Amesema serikali inafuatilia kwa karibu kampeni zinazoendelea ili kuhakikisha kuwa inazuia kutokea kwa vurugu.

  Serikali ya Kenya imetambua baadhi ya maeneo yenye uwezekano wa kutokea vurugu na kuchukua hatua za kuzuia kutokea kwa vurugu kwenye maeneo hayo.

  Bw Nkaissery amesema serikali imehamasisha wanasiasa, mashirika na hata jamii kufanya kampeni za amani na kuhimiza watu kuishi kwa masikilizano.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako