• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la ukanda mmoja, njia moja laweka njia wazi ya mustakbali wa ushirikiano

    (GMT+08:00) 2017-05-18 09:16:50

    Mjumbe wa taifa wa China Bw Yang Jiechi amesema mkutano uliofungwa hivi karibuni wa Baraza la ushirikiano wa kimataifa la ukanda mmoja na njia moja, umetoa mwongozo wa mafanikio na kuweka wazi njia ya mwelekeo wa ushirikiano.

    Bw Yang amesema mkutano huo ulikuwa ni shughuli kubwa ya kidiplomasia kupendekezwa na kuandaliwa na China tangu kuanzishwa kwa jamhuri ya watu wa China. Amesema kwenye kuandaa mkutano huo China haikuwa na nia za ubinafsi za kujitafutia maslahi binafsi, na iliandaa mkutano huo kwa mtazamo wazi, shirikishi, na wa kidemokrasia.

    Viongozi 29 wa nchi na serikali walihudhuria mkutano huo, ikiwa ni pamoja na maofisa wa serikali, wafanya biashara, wahisani na wanahabari kutoka zaidi ya nchi 130.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako