Bw Barnier amemtaka waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May kuendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya wakati pande hizo zinafanya mazungumzo badala ya kupingana na kutarajia kufikia makubaliano na Uingereza.
Bibi Theresa May aliuandikia barua Umoja wa Ulaya mwezi wa Machi na kuanzisha rasmi mchakato wa Uingereza kujitoa umoja wa Ulaya, mchakato ambao utamalizika mwezi wa Machi mwaka kesho. Mazungumzo husika yataanzishwa baada ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utakayofanyika tarehe 8 mwezi ujao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |