• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • King Power International kuinunua klabu ya OH Leuven ya Ubegiji

    (GMT+08:00) 2017-05-18 09:37:25

    Wamiliki wa Leicester City, King Power International wamekubali kuinunua klabu ya OH Leuven ya Ubegiji. Klabu hiyo daraja la pili iliyoko mashariki mwa mji wa Brussels, iliepuka kushushwa daraja msimu huu. Bodi ya klabu hiyo awali ilikuwa ikitafuta wawekezaji na King Power ndio waliokuwa wametuma ombi la zabuni kwa uwazi .

    Wakurugenzi wake walisema mkataba huo utaiwezesha kifedha na katika vigezo vya mchezo. OH Leuven walishushwa daraja kutoka ligi ya dara la kwanza ya Ubegiji mwaka 2015-16 lakini wamesema umiliki mpya utawapa ufadhili wa kifedha unaotosha kama njia ya kuwasaidia kurudi katika ligi ya dara la kwanza.

    Imeongeza kwamba King Power, iliyoanzishwa na mwenyekiti wa Leicester Vichai Srivaddhanaprabha mwaka 1989 itafadhili upanuzi wa mfumo wa klabu ya vijana. Ununuzi huo utakamilishwa rasmi wakati kampuni itapokamilisha mkataba huo. Srivaddhanaprabha anakadiriwa kuwa na utajiri wathamani ya £3.6bn kulingana na jarida la Forbes

    Mwenyekiti huyo mwenye umri wa miaka 58 aliinunua Leicester mwaka 2010, ambapo klabu hiyo ilifanikiwa kupanda hadi katika ligi kuu ya Uingereza miaka minne baadaye na kujinyakulia taji la ligi kuu ya Uingereza 2015-16.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako