• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Cesc Fabregas aahidi kuizamisha Arsenal itakapokutana na Chelsea

    (GMT+08:00) 2017-05-18 09:37:44

    Mchezaji wa zamani wa Arsenal Cesc Fabregas baada ya kuhamia katika timu ya Chelsea anasema kuwa wakati timu hizo mbili zitakutana katika mchuano wa fainali ya kombe la FA Mei 27, atahakikisha anaizamisha timu yake hiyo ya zamani. Baada ya kuwa na Arsenal kwa misimu minne mfululizo, aliondoka kwenda kusakata gozi katika Klabu cha Barcelona mwaka wa 2011.

    Mchuano huo ambao utasakatwa katika uwanja wa Wembley utakuwa wa kuwapa Arsenal inayofunzwa na Arsene Wenger mwanya wa kupata taji la kujituliza msimu huu baada ya kujikuta wakiwa hawana uwezo tena wa kuinua taji kwa niaba ya mashabiki wao.

    Kwa sasa, Arsenal inakimbizana na mwanya unaotegemea muujiza kumaliza katika nafasi ya nne katika ligi kuu ya Uingereza na kujihakikishia uwezekano wa kushiriki dimba la Klabu Bingwa Barani Ulaya. Matumaini hayo yanategemea matokeo ya mchuano wa mwisho Jumapili kati yake na Everton na pia matokeo dhidi ya Liverpool na Middleborough.

    Kwa mujibu wa Ferbregas, Chelsea iko tayari na ina ari kuu ya kumnyima Wenger uwezekano wa kuvunja rekodi ya kutwaa kombe hilo zaidi ya mara sita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako