• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SportPesa yaingia mkataba wa udhamini na klabu ya Yanga SC

    (GMT+08:00) 2017-05-18 09:38:05

    Kampuni ya michezo ya kubashiri nchini Tanzania, SportPesa jana iliingia mkataba wa udhamini na klabu ya Yanga SC wenye thamani ya Shilingi billioni 5.22 kwa kipindi cha miaka mitano zaidi ya mahasimu wao, wekundu wa Msimbazi Simba SC. Yanga inakua ni klabu ya pili nchini kulamba udhamini huo ikiwa ni baada ya watani wao wajadi Simba kufanya hivyo juma moja kupita dau la Shilingi Bilioni 4.96.

    Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba huo makao makuu ya Yanga, Mkurugenzi wa Utawala wa SportPesa, Tarimba Abbas amesema wameingia udhamini na klabu hiyo kwa dhumuni la kuendeleza soka katika kufikia malengo waliyojiwekea.

    Kwa mara nyingine tena, mahasimu hao wa jadi Simba na Yanga wanatarajiwa kuwa chini ya udhamini mmoja tena.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako