• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maafisa wa NOCK ya Kenya washitakiwa kwa wizi

    (GMT+08:00) 2017-05-18 09:38:47

    Wasimamizi wa Kamati ya Olimpiki nchini Kenya, NOCK, wameshtakiwa kwa njama za wizi na usimamizi mbaya wa fedha na sare za kikosi cha Kenya katika mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika mjini Rio, Brazil mwaka uliopita.

    Ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka nchini Kenya, ODPP imetangaza kuwa, baada ya kutathmini uchunguzi, maafisa hao wanastahili kushtakiwa kwa makosa hayo. Wasimamizi hao wakiwemo msimamizi wa timu ya Kenya kwenye Olimpiki, Stephen Soi, aliyekuwa naibu mkuu wa ujumbe wa Olimpiki, Bernard Ekumbo, katibu mkuu, FK Paul na naibu meneja wa timu hiyo, Pius Ochieng watafikishwa mahakamani baadaye mwezi huu kujua hatma yao.

    Mwaka uliopita, maafisa wa polisi walinasa sare za wanariadha katika makazi ya naibu mwenyekiti, Ben Ekumbo kufuatia malalamiko ya wanariadha kuwa hawakupokea sare za kutosha. Aidha, baadhi ya maafisa wengine wa kikosi cha Kenya kwenye Olimpiki, walieleza kudhalilishwa katika mashindano hayo kwa kutopewa makazi mjini Rio na kuishi katika hali duni.

    Kikosi cha Kenya kilikumbwa na sakata mbalimbali licha ya kuandikisha matokeo mazuri kwenye mashindano ya Olimpiki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako