• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China, UNICEF na UNFPA kuzidisha ushirikiano chini ya mpango wa "Ukanda mmoja na Njia Moja"

    (GMT+08:00) 2017-05-18 09:39:44

    Naibu waziri mkuu wa China Bibi Liu Yandong amesema China itaongeza ushirikiano na Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, na Shirika la idadi ya watu la Umoja wa Mataifa UNFPA chini ya mpango wa "Ukanda mmoja na Njia moja".

    Bibi Liu Yandong kwa nyakati tofauti alikutana na mkurugenzi mtendaji wa UNICEF Bw. Anthony Lake na mkurugenzi mtendaji wa UNFPA Babatunde Osotimehin, waliokuwa mjini Beijing kuhudhuria mkutano wa kilele wa baraza la "Ukanda mmoja na Njia Moja".

    Bibi Liu Yandong pia amehakikisha kuwepo kwa ushirikiano halisi na wa muda mrefu, kati ya China na mashirika hayo mawili ya Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako