• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni za China zafungua nafasi za ajira Kenya

  (GMT+08:00) 2017-05-18 09:53:00

  Kuendelea kuongezeka kwa uwekezaji wa kampuni za China nchini Kenya kumesaidia kupunguza ukosefu wa ajira hasa kwa vijana. Kulingana na taakwimu hadi sasa nchini Kenya kuna zaidi ya kampuni 300 za China kwenye sekta za ujenzi, utengenezaji bidhaa, na utoaji huduma zote zikitoa ajira kwa wakenya. Taakwimu zinaonyesha kwamba karibu kila kampuni ya China inaajiri asilimia 70 ya wenyeji.

  Kampuni ya China Wuyi imewekeza dola milioni 100 kujena kiwanda hiki ambacho ni sehemu ya makubaliano ya Ukanda mmoja na Njia moja yaliotiwa saini na Rais wa China Xi Jinping na mwezake wa Kenya Uhuru Kenyatta. Kwa sasa zaidi ya wenyeji 500 wameajiriwa hapa.

  Bwana John Owino ni mhadisi kwenye kampuni hii ya China Wuyi precast.

  "Kitu ya kwanza tunapokuja ni kuhakikisha mashine ziko sawa na pia kupanga watu kwa kazi za siku. Hii teknolojia ni zuri sana, tunatengeneza paneli za nyumba na hapa kuna mashine moja ya kisasa zaidi ambayo ni ya kipekee katika kanda ya afrika mashariki na kati"

  Kilomita 50 kutoka hapa ni kampuni ya Twyford ya kutengeneza vigae ilioanzishwa miezi sita tu iliopita. Ikiwa imewekeza kwenye teknolojia ya kisasa kampuni hii ya China inatarajia kuongeza mgao wa soko lake kutoka 60 hadi 70 ndani ya miaka miwili. Hapa pia ni mfano mwingine wa vile kampuni za China zinasaidia kufungua nafasi za ajira.

  Bwana Li Ruiqin ni meneja mkurungezi.

  "Wenyeji wanafanya kazi za uchukuzi, kuchimbua mali ghafi, na pia kwenye nafasi za usimamizi. Baadaye tutafanya upanuzi na kuzalisha mita za mraba 60,000 za vigae kwenye laini ya kwanza na ya pili, wakati huo tutaajiri watu 1,500".

  Kampuni hii ambayo ni ushirikiano kati ya ile ya Sunda International Group na Keda Clean Energy sasa imeajiri wenyeji 600. Aidha inatumia maligafi za hapa kuzalisha bidhaa zake na hivyo kuifanya bei kuwa nafuu.

  Bwana Alan Ogeto ni mkuu wa raslimali watu kwenye kampuni hii.

  "Tumeajiri watu wa Kenya 600 na tuna vitengo kama vile gas station ambayo iko na karibu wafanyakazi 50 kuna sehemu ya mali gafi na sehemu ya uchapishaji. Mimi binafsi nimefurahia teknolojia ya kutoka nje ambayo sasa imesaida eneo hili kufunguka kiviwanda"

  Kwa jumla Twyford inaweza kuzalisha aina yoyote ya vigae kulingana na mahitaji ya wateja. Pia wanaweza kuchapicha picha zozote kwenye vigae.

  Nicodemus ni msimazi wa ubora wa bidhaa.

  "Mimi ni msimamizi na mdhibiti wa ubora kwenye hii kampuni, naangalia kama bidhaa zimefikiwa viwango vinavyohitajika kwa ukubwa upana na kila hali. Pia naangalia kama zina nyufa au mashimo. Wachina ni wazuri sana ile kitu wanataka sana ni kuelewana . Tuna changamoto kidogo ya lugha lakini tunajaribu vile tunaweza kuelewana"

  Kupanda kwa mahitaji ya nyumba kwenye miji ya Nairobi Mombasa na Kisumu kunamaanisha pia mahitaji ya vifaa vya ujenzi pia yamepanda. Lakini ujio wa kampuni kama hizi za china unahakikisha siku za mbele kwenye sekta ya ujenzi ni zenye matumaini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako