• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mafanikio yaliyopatikana katika kupunguza umaskini katika miaka ya hivi karibuni nchini China

  (GMT+08:00) 2017-05-18 19:00:28

  Umaskini ni tatizo kubwa linalokabili dunia nzima. Takwimu zilizotolewa mwaka 2016 na Benki ya Dunia zimeonesha kuwa, hivi sasa duniani kuna watu maskini milioni 700. China ikiwa nchi kubwa zaidi inayoendelea, ingawa idadi ya watu wake maskini imepungua kutoka milioni 82 ya mwaka 2012 hadi milioni 40 ya hivi sasa, lakini lengo la serikali ya China ni kutokomeza kabisa tatizo la umaskini kabla ya mwaka 2020. Ili kutimiza lengo hilo, rais Xi Jinping wa China imeagiza kuchukua hatua halisi zenye ufanisi kuhusu suala hilo.

  Katika kijiji cha Ma'erzhuang kilichoko Wilaya ya Yanchi katika Mkoa unaojiendesha wa Ningxia, China, magari mengi yameegeshwa mbele ya nyumba mbalimbali.

  Lu Wentao ni mwanakijiji wa kijiji hicho. Katika miaka mingi iliyopita, alikuwa amefanya kazi ya vibarua nje ya kijiji hicho, na kujishughulisha na uuzaji wa nguo, na ufugaji wa mifugo. Alirudi kijiji kwake mwaka 2010, na kuanza kufuga mbuzi a aina ya Yanchitan ambao wanajulikana sana katika sehemu ya huko, na kujiunga na jumuiya ya wafugaji ya kijiji hicho. Lu Wentao ameeleza kuwa, mapato yake kutokana na kuuza mbuzi kwa maka ni Yuan laki 2.

  "Sasa unafuga mbuzi waangapi?"

  "zaidi ya 7,000, kila ninaponunua mbuzi wapya, wanapimwa na daktari wa wanyama."

  "kila mbuzi ni Bei gani?"

  "Hivi sasa wanauzwa kwa yuan 42 kwa kilo. Pia tunapewa ruzuku kutoka serikali kutokana na kufuga na mbuzi wa aina hiyo."

  Kijiji cha Ma'erzhuang kiko katika sehemu ya Jangwa ya Maowusu na Uwanda wa Juu wa Huangtu iliyoko kaskazini magharibi nchini China, na mbuzi wa aina ya Yanchi ni bidhaa yenye umaalumu wa huko, na iliandaliwa kwa ajili ya Michezo ya OlimpikI ya Biejing. Na wanakijiji wa huko walikuwa wanaishi kwa kutegemea kufuga mbuzi, lakini kila majira yanapobadilika, na magonjwa yanaibuka, na faida ya ufugaji wa mbuzi inapungua. Mkuu wa kijiji hicho Feng Lizhen amesema maisha ya wanakijiji katika miaka mingi iliyopita yalikuwa magumu.

  Katika miaka mingi iliyopita, wanakijiji wa Ma'erzhuang walianzisha viwanda vyenye umaalumu vya ufugaji, ambapo wafugaji wanaweza kufundishana uzoefu wa ufugaji, na jamii ya ushirikiano inashughulikia kutafuta njia za kuuza. Mwaka 2016, vyakula vilivyopikwa kwa kutumia nyama ya mbuzi ya "Yanchitan" viliandaliwa kwa ajili ya Mkutano wa viongozi wa G20 uliofanyika mjini Hangzhou, na mwaka huo familia 59 kati ya 64 zilizothibitishwa na Kijiji cha Ma'erzhuang zilikuwa zimeondokana na umaskini, na wastani wa mapato ya wanakijiji ulifikia yuan 8,500 kwa mwaka, na theluthi ya mapato hayo yanatokana na ufugaji wa mbuzi. Feng Lizhen anasema, hivi sasa bado kuna familia 5 ambazo hazijaondokana na umaskini, na chanzo kubwa ni kutokana na magonjwa au ukosefu wa nguvu kazi.

  Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya China katika ngazi mbalimbali imetangaza sera mfululizo ili kuvisaidia vijiji na watu maskini kuendeleza kilimo, ufugaji na utengenezaji kwa mikono. Kutokana na hatua hizo, vijiji vingi kama kijiji cha Ma'erzhuang vimeondokana na umaskini. Idadi ya watu maskini imepungua kutoka milioni 82 ya mwishoni mwa mwaka 2012 hadi milioni 40 ya mwaka jana. Mwezi Machi mwaka huu, serikali ya China imetangaza tena lengo la kupunguza idadi ya watu maskini kwa milioni 10 ndani ya mwaka huu, na kutimiza kuondoa watu maskini wote ifikapo mwaka 2020.

  Aliyekuwa mkurugenzi wa Shirika la Mipango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bi Helen Clark alieleza kuwa, China imepata mafanikio makubwa katika kutimiza malengo ya maendeleo ya Milenia, na kuwasaidia watu zaidi ya milioni 100 kuondokana na umaskini, uzoefu huu i unaoweza kuigwa na dunia nzima. Waziri wa zamani wa Jamhuri ya Czech hivi karibuni pia anasema:

  "Nchini China, watu zaidi ya milioni 100 wameondokana na umaskini, na lengo hili lilitimizwa ndani ya muda mfupi, ni mafanikio ambayo hapo zamani hayakupatikana. Katika miongo kadhaa iliyopita, watu zaidi ya milioni 800 wamedoka kwenye tatizo hilo na kupata dola 9 za kimarekani kwa siku. Hayo yametokana na ongezeko la kasi la uchumi wa China."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako