• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa wito kuongeza misaada kwa Somalia

  (GMT+08:00) 2017-05-18 19:03:06

  Naibu balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Wu Haitao amesema, jumuiya ya kimataifa inapaswa kuendelea kuongeza ufuatiliaji na nguvu ya misaada kwa Somalia ili kuisaidia kudumisha utulivu na maendeleo ya uchumi.

  Bw. Wu amesema, hivi sasa, Somalia inakabiliana na changamoto za kisiasa, usalama, uchumi na haki za binadamu. Amesema watu milioni 6.2 nchini Somalia wanakosa chakula, miongoni mwao, karibu milioni 3 wanahitaji msaada wa dharura wa chakula.

  Bw. Wu pia amesema, China inaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Somalia katika kupata amani na maendeleo na inapenda kushiriki kwenye mchakato wa amani wa Somalia na kusukuma mbele utatuzi wa kisiasa wa mgogoro nchini humo kwa ajili ya amani, utulivu na maendeleo ya eneo la Pembe ya Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako