• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Uchumi wa Rwanda kukua kwa asilimia 6.2 mwaka huu

    (GMT+08:00) 2017-05-18 19:07:58

    Uchumi wa Rwanda unatarajiwa kukua kwa asilimia 6.2 mwaka huu hasa ukisaidiwa na kupanuka kwa sekta ya kilimo na mauzo ya nje ya nchi.

    Shirika la fedha duniani limesema kufuatia msimu mzuri wa mvua bei ya vyakula haitapanda na mfumko wa bei utaendelea kushuka.

    Aidha kahawa na chai ambazo huuzwa nje zinatarajiwa kufanya vizuri.

    Kampeni ya Made-in-Rwanda pia inatarajiwa kuchangia ukuaji huo.

    IMF imesema mwanya wa kibiashara wa asilimia 17 uliokuwepo mwaka 2016 pia umepungua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako