• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Bei ya mazao ya chakula Tanzania yaongezeka kwa asilimia 56.

    (GMT+08:00) 2017-05-18 19:12:07

    Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji nchini Tanzania imesema bei ya mazao ya chakula nchini imeongezeka kwa asilimia 56.

    Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage alisema wakati akisoma bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2017/18.

    Alisema gunia moja la mahindi lenye uzito wa kilo 100 limepanda kutoka Sh59,873 katika msimu wa mwaka 2015/16 hadi kufikia Sh 99, 527 kwa msimu wa 2016/17 sawa na asilimia 66.23.

    Alisema bei za mazao makuu ya chakula kama vile mahindi, maharagwe, mchele, ngano, uwele, ulezi na mtama zimeongezeka kwa kiwango tofautitofauti.

    Alisema bei ya mchele kwa gunia la kilo 100 iliongezeka kutoka wastani wa Sh177,340 msimu wa mwaka 2015/16 hadi kufikia Sh191,289 msimu wa 2016/17.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako