• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Kampuni ya madini ya Acacia kupunguza wafanyakazi zaidi ya 100

    (GMT+08:00) 2017-05-18 19:14:57

    Kampuni ya Acacia, inayomiliki mgodi wa Buzwagi, imetengaza kupunguza wafanyakazi zaidi ya 100 wakati ikijiandaa kufunga mgodi huo ifikapo mwaka 2020.

    Meneja mahusiano wa kampuni hiyo, Nector Foya amesema taarifa ya kupunguza wafanyakazi ilitolewa baada ya meneja mkuu wa Buzwagi, Stewart Hamilton kuzungumza na wafanyakazi wa mgodi huo jana.

    Taarifa hiyo inaeleza kuwa wafanyakazi 100 watapunguzwa baada ya kufanyika vikao mbalimbali katika wiki mbili, kuanzia jana ikiwa ni pamoja na kujibu maswali mbalimbali.

    Mbali na upunguzwaji huo, taarifa inaeleza kuwa wafanyakazi hao watatoka katika idara zinazotoa msaada na huduma.

    Aidha taarifa inaeleza kuwa uchimbaji wa mgodi huo utaanza kumalizikia katika robo ya nne ya mwaka na uchimbaji utaishia mwisho wa Desemba 2017 na uchenjuaji utaisha 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako