• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Japan na mjumbe maalum wa Korea Kusini wakubali kurejesha ushirikiano wa kidiplomasia

    (GMT+08:00) 2017-05-18 19:27:48

    Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe na mjumbe maalum wa rais mpya wa Korea Kusini Moon Hee-sang wamekubaliana kurejesha ushirikiano wa kidiplomasia kati ya viongozi wa nchi hizo.

    Katika mazungumzo kati ya viongozi hao yaliyofanyika Tokyo hii leo, waziri mkuu Abe na mjumbe wa rais wa Korea Kusini Moon Hee-sang, walirudia ahadi iliyowekwa na Abe na rais Moon Jae-in wa Korea Kusini katika mzungumzo yao ya simu baada ya rais mpya wa Korea Kusini kuapishwa hivi karibuni.

    Ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Japan na Korea Kusini awali ulishuhudia viongozi wa nchi hizo wakitembeleana mara moja kwa mwaka, lakini majadiliano hayo yalisitishwa tangu mwisho wa mwaka 2011 na utawala wa wakati huo wa rais Lee Myung Bak.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako