Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni mkurugenzi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja huo Bw. Michael Sidibe amesema Umoja wa Mataifa unatumia uzoefu wa China katika kupanga kuwafundisha wafanyakazi milioni 2 wa afya barani Afrika.
Bw. Sidibe amesema uzoefu wa miaka mingi wa China umethibitisha kuwa madaktari wanaowasaidia wakulima vijijini ni nyongeza nzuri ya madaktari maalumu. Amesema madaktari hao wamekuwa sehemu muhimu katika jamii na mashirika ya afya, hasa kwenye maeneo ya kijijini ambapo hali ya matibabu iko nyuma.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |