• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bw. Yang Jiechi aeleza mafanikio ya Baraza la Kimataifa la Ushirikiano la "Ukanda Mmoja, Njia Moja"

  (GMT+08:00) 2017-05-18 20:14:26
  Bw. Yang Jiechi aeleza mafanikio ya Baraza la Kimataifa la Ushirikiano la "Ukanda Mmoja, Njia Moja"

  Mjumbe wa taifa wa China Bw. Yang Jiechi ameongelea mafanikio yaliyopatikana katika Mkutano wa kilele wa Baraza la Kimataifa la Ushirikiano la "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

  Akizungumza na waandishi wa habari hii leo, Bw. Yang amesema, mkutano huo umeamua upande wa kufanya ushirikiano kwa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" katika siku za baadae, kuweka mipango halisi ya ujenzi wa mpango huo, na kuthibitisha miradi muhimu itakayotekelezwa.

  Amesema kazi kuu inayofuata ni kuanzisha uhusiano wa aina mpya wa kimataifa, na kujenga uhusiano wa kiwenzi wa kutopambana na kutofungamana na upande wowote; kukuza ushirikiano na mawasiliano ya viwanda, na kukamilisha utaratibu wa dhamana ya fedha. Pia kutimiza utandawazi wa dunia ulio wa wazi, shirikishi, kunufaisha pande zote, na kuleta faida za pamoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako