• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hatua ya Japan ya kuongeza hali ya wasiwasi ya Bahari ya Kusini haitasaidia amani na utulivu ya sehemu hiyo

    (GMT+08:00) 2017-05-18 20:17:46

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Hua Chunying amesema, China inahimiza Japan kuchukua msimamo sahihi na kuhimiza kuaminiana kati ya nchi mbalimbali kuhusu Bahari ya Kusini ya China.

    Bi. Hua amesema hayo kutokana na kauli iliyotolewa na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe na waziri mkuu wa New Zealand Bill English ambaye yuko ziarani nchini Japan kuhusu ufuatiliaji wa Bahari ya Kusini, na kuzitaka pande zote zisichukue hatua za uchokozi.

    Bi Hua Chunying amesisitiza kuwa, kutokana na juhudi za pamoja za China na nchi zilizo pwani ya Bahari ya Kusini, hali ya sehemu hiyo imeboreshwa, na taarifa hiyo ya pamoja imetolewa kwa wakati usio mwafaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako