• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • AS Monaco yatwaa taji la ligi Ufaransa

  (GMT+08:00) 2017-05-19 08:56:05
  Klabu ya AS Monaco ya nchini Ufaransa juzi wametwaa taji la ligi hiyo kwa mara ya kwanza, tangu wafanye hivyo miaka 17 iliyopita, ushindi wao wa magoli 2 kwa 0 walioupata nyumbani dhidi ya klabu ya Saint-Etienne uliwatosha kabisa kutangaza ubingwa msimu huu.

  Kwa ushindi huo umewafanya wababe wa ligi hiyo ya Ufaransa klabu ya Paris St-Germain kuondolewa katika kinyang'anyiro hicho msimu huu kwa kuzidiwa alama tatu dhidi ya vinara hao na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.

  Klabu hiyo imeonekana kuwa na wachezaji vijana na hivyo mafanikio yao yanakwenda sawia na umri wao, kwani mara ya mwisho Monaco kushinda taji hilo la ligi walikuwepo wachezaji wa kifaransa kama Fabien Barthez, David Trezeguet pamoja na Willy Sagnol.

  Mafanikio ya AS Monaco msimu huu ni makubwa mnoo ambayo yamechangiwa na wachezaji kama Falcao raia wa Colombia na kijana mdogo wa kifaransa, Mbappe.

  Falcao, mwenye umri wa miaka 31, hakuwa na msimu mzuri alipokuwa katika klabu ya Manchester United pamoja na Chelsea, ambapo alishinda magoli matano tu katika michezo yake 36 aliyoingia uwanjani.

  Nahodha huyo wa Monaco sasa ameshinda jumla ya magoli 24 na kuchangia pasi 4 zilizo zalisha magoli.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako