• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya kutumia utafiti na teknolojia kufikia malengo ya maendeleo ya Umoja wa mataifa

  (GMT+08:00) 2017-05-19 08:58:01

  Kenya inaendelea na mchakato wa kupokea sayansi na teknolojia ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya umoja wa mataifa.

  Mkurugenzi wa kamati ya sayansi, teknolojia na uvumbuzi ya Kenya Bw Moses Rugut amesema madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa yanayoikumba Kenya, yanaweza kupunguzwa kwa kutumia sayansi na teknolojia. Amesema kamati yake inatafuta njia za kuleta suluhisho la kudumu la matatizo ya ukame, mafuriko na maji, ikiwa ni pamoja na kutafuta uwezekano wa kupanda mazao yanayohimili ukame ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa chakula.

  Bw Rugut amesema hayo wakati wiki ijayo Kenya itakuwa mwenyeji wa mkutano wa wiki ya sita ya sayansi, utakaohudhuriwa na wajumbe wa kikanda na wa kimataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako