• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Russia yasema hakuna siri zilizovujishwa na Rais Trump kwa waziri wake wa mambo ya nje

  (GMT+08:00) 2017-05-19 08:58:51

  Waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw Sergei Lavrov amesema habari kuwa Rais Donald Trump wa Marekani alimpa siri za Marekani alipokutana naye kwenye ikulu ya Marekani si za kweli.

  Bw Lavrov amesema alichoambiwa na Rais Trump ni kuwa kundi la IS linaweza kuweka mabomu yasiyogundulika kwenye kompyuta za Laptop. Amesema habari hiyo ilitangazwa miezi miwili au mitatu iliyopita na haoni kuwa hiyo ni siri.

  Kauli ya Bw Lavrov ni ya kwanza kutolewa hadharani tangu vyombo vya habari viripoti kuwa maofisa wawili wa Marekani wamesema Rais Trump alivujisha siri za Marekani kwa Bw Lavrov walipokutana kwenye Ikulu ya Marekani.

  Bw Lavrov pia amezungumzia suala la uhusiano kati ya Umoja wa Ulaya na Russia, na kusema hali ya sasa vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa Ulaya kwa Russia kutokana na suala la Ukraine, haviunufaishi upande wowote, na Russia ingependa kuboresha uhusiano kati yake na Umoja wa Ulaya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako