• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • ECA yahimiza nchi za Afrika kufanya mageuzi ya kiuchumi ya kiviwanda

  (GMT+08:00) 2017-05-19 09:20:49

  Kamati ya uchumi ya Umoja wa Mataifa kanda ya Afrika ECA imesisitiza kuwa mageuzi ya uchumi ya Afrika yanapaswa kufuatilia sekta ya viwanda ili kupata maendeleo endelevu na ya pande zote barani humo.

  Katibu mtendaji wa kamati hiyo Abdalla Hamdok amesema, katika miaka sita iliyopita, ECA imefuatilia juhudi zilizofanywa kwa ajili ya kuunga mkono ajenda ya viwanda ya Afrika, na bara hilo litanufaika katika kupambana na umaskini, ukosefu wa usawa na ukosefu wa ajira kwa kupitia mchakato wa kuendeleza viwanda.

  Bw. Hamdok aliyasema hayo jana kwenye ufunguzi wa Kikao cha tatu cha baraza la maendeleo endelevu barani Afrika kitakachofanyika kwa siku mbili. Ameongeza kuwa mafunzo yanapaswa kupatikana kupitia uzoefu wa mafanikio kutoka nchi nyingine kama China, ambayo amesema imepiga hatua kubwa katika kupunguza umaskini kupitia kuendeleza viwanda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako