• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shambulizi la gari kuparamia watu lasababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 22 kujeruhiwa New York

  (GMT+08:00) 2017-05-19 09:29:47

  Shmabulizi la gari kuparamia watu limetokea jana kwenye uwanja wa Times Square mjini New York, Marekani, na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 22 kujeruhiwa.

  Meya wa mji wa New York Bw Bill De Blasio amesema hadi sasa hakuna uthibitisho kuwa tukio hilo linahusiana na ugaidi, lakini polisi ya New York imeimarisha hatua za kiusalama dhidi ya ugaidi mjini humo.

  Kamishna wa polisi wa New York Bw James O'Neal amesema dereva mwanaume, alikuwa ameendesha gari kwenye njia ya waenda kwa miguu na kugonga nguzo ya barabara, mwanamke mmoja amefariki na wengine 22 wamejeruhiwa. Dereva huyo ametiwa mbaroni kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako