• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Kenya kununua gunia la mahindi kwa shilingi 3600

  (GMT+08:00) 2017-05-19 19:34:12

  Serikali ya Kenya imesema iko tayari kununua mahindi kutoka kwa wakulima kwa shilingi 3600 badala ya bei ya awali ya shilingi 3000 kwa gunia la kilo 90 ili kuongeza kiwango cha mahindi katika maghala yake. Akizungumza na radio China kimataifa, waziri wa kilimo wa Kenya Bwana Willy Bett amesema serikali imegundua kuwa wakulima bado wanahifadhi takriban magunia milioni 4 ya mahindi huku kukiwa na uhaba wa mahindi kote nchini Kenya. Kauli hiyo ya Bett inakuja wakati ambapo kumekuwa na shinikizo kutoka kwa wabunge wa Kenya waliodai mpango wa kuagiza mahindi kutoka nje utawafaidi wafanyabiashara na wasagaji huku wakulima wakiumia. Bwana Bett amesema hivi sasa kuna magunia 980,000 ya mahindi pekee ilhali wakenya wanatumia magunia milioni 3 kila mwezi. Wiki jana, magunia laki 3 yaliingizwa nchini Kenya kutoka Mexico ili kufidia uhaba unaoshuhudiwa nchini wakati huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako