• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wabunge waitaka serikali ya Magufuli kuweka utaratibu usio na urasimu

  (GMT+08:00) 2017-05-19 19:34:36

  Serikali ya Tanzania imetakiwa kuweka kuweka utaratibu usio na urasimu kwa wawekezaji. Wabunge wa Tanzania wamesema hatua hiyo inatokana na utaratibu wa sasa kuwa na vikwazo vingi vinavyokimbiza wawekezaji.

  Aidha, wabunge hao pia wameishauri serikali kutumia vyema rasilimali na malighafi zilizopo katika kuijenga sekta hiyo ya viwanda ili mafanikio ya viwanda hivyo yasiishie tu kwenye kuongeza ajira bali kuinua uchumi na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

  Wabunge hao, wameitaka serikali kuanzisha kituo kimoja (one Stop center) kwa ajili ya kutoa huduma zote katika sehemu moja kwa wawekezaji jambo litakaloongeza vivutio kwa uwekezaji lakini pia kuwarahisishia wawekezaji hao kufanikisha kiurahisi taratibu za kuwekeza nchini.

  Kauli hiyo inakuja wakati ambapo ripoti zinaonesha kuwa uzalishaji viwandani umeshuka kutoka dola za kimarekani milioni 1.4 mpaka dola za 870,000.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako