• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima Kenya waitaka serikali kutangaza majina ya wanaoagiza sukari

    (GMT+08:00) 2017-05-19 19:35:14

    Wakulima wa miwa nchini Kenya wameitaka serikali kutangaza kampuni ambazo zimepewa leseni ya kuagiza sukari kutoka nje. Wakulima hao wamesema ijapokuwa kiwango cha sukari kinachozalishwa Kenya hakitoshi uagizaji wa bidhaa hiyo unatakiwa kufanywa kwa utaratibu utakaohusisha wadau.Katibu mkuu wa chama cha wakulima wa miwa Kenya Bwana Francis Wangara ameitaka serikali kufutilia mbali uamuzi huo hadi pale shaka waliyonalo itakapoangaliwa na serikali. Wangara amesema kunja zaidi ya kampuni 50 ambazo ziliwasilisha ombi la kuagiza sukari kutoka nje bila kulipa ushuru. Chama hicho kimesema kina hofu kuwa sukari inayozalishwa nchini Kenya haitaweza kumudu ushindani kama hali itaendelea kuwa hivo. Wameitaka serikali kuwa wazi kwa kila kitu ikiwemo tani zinazoagizwa na kampuni husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako