• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na mjumbe maalumu wa Korea ya Kusini

    (GMT+08:00) 2017-05-19 19:39:33

    Rais Xi Jinping wa China leo amekutana na mjumbe maalumu wa Korea ya Kusini Bw. Lee Hai-chan katika Jumba la mikutano ya Umma mjini Beijing.

    Katika mazungumzo hayo, rais Xi amesema hivi sasa uhusiano kati ya China na Korea ya Kusini uko katika kipindi muhimu, na kusisitiza kuwa China inashikilia kutimiza Peninsula ya Korea isiyo na silaha za nyuklia. Pia kulinda amani na utulivu katika peninsula hiyo, na kushikilia kutatua masuala ya peninsula hiyo kwa njia ya mazungumzo, mambo yanalingana na maslahi ya pamoja ya China na Korea ya Kusini na sehemu hiyo.

    Bw. Lee Hai-chan amesema Korea ya Kusini inafahamu ufuatiliaji mkubwa wa China, pia inapenda kuimarisha mawasiliano na uratibu katik ya nchi hizo na kujadiliana njia mwafaka ya kutatua matatizo yanayoyakwamisha maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako