• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Kagame wa Rwanda ajiandaa kustaafu mwaka 2024

  (GMT+08:00) 2017-05-19 20:33:06

  Gazeti la The New Times la Rwanda leo limeripoti kuwa, rais Paul Kagame wa nchi hiyo hivi karibuni alidokeza kuwa, kama atashinda tena katika uchaguzi mkuu wa urais utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu, atastaafu baada ya kumaliza kwa muda wake mwaka 2024.

  Rais huyo mwenye miaka 59 amesema hayo alipofanya mahojiano na mwandishi wa habari wa gazeti la Ufaransa Jeune Afrique. Amesema chama tawala cha nchi hiyo FPR na wananchi wake wanatarajia kuwa ataendelea kushika madaraka ya urais baada ya uchaguzi huo, lakini atafahamisha msimamo wake kwa wafuasi wake wakati kampeni za uchaguzi mkuu zitakapoanza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako