• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mazungumzo ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa yapata mafanikio halisi

  (GMT+08:00) 2017-05-19 21:10:35

  Mkuu wa ujumbe wa China ambaye pia ni naibu mkuu wa idara ya kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Lu Xinming amesema kuwa ya duru ya kwanza ya mwaka 2017 ya mazungumzo ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa imemalizika jana huko Bonn, nchini Ujerumani na kupata mafanikio makubwa.

  Bw. Lu Xinming amesema mkutano huo umefikia maoni ya pamoja kuhusu utekelezaji wa makubaliano ya Paris yaliyofikiwa mwezi Novemba mwaka jana, ambayo yanatoa mpango wa vitendo wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa baada ya mwaka 2020. Lakini bado kuna maoni ya tofauti katika mazungumzo hayo, yakiwemo kutofautisha majukumu ya nchi zilizoendelea na nchi zinazoendelea na jinsi zitakavyohakikisha kuhimiza mazungumzo kwa pande zote na kwa uwiano.

  Aidha katibu mtendaji wa kanuni ya mpango wa mabadiliko ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa Bw. Patricia Espinosa amezitaka pande zote zilizosaini kanuni hiyo kutekeleza ahadi na kulinda makubaliano ya Paris.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako