• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe mambo ya nje wa China ampigia simu waziri wa mambo ya nje wa Marekani

    (GMT+08:00) 2017-05-20 18:40:23

    Mjumbe wa mambo ya taifa wa China Bw. Yang Jiechi amempigia simu waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Rex Tillerson.

    Bw. Yang amesema baada ya rais Xi Jinping na rais Donald Trump kukutana huko Mar-a-Lago, uhusiano kati ya China na Marekani umepata maendeleo mazuri. Katika kipindi kijacho, pande mbili zitaendelea kutekeleza maoni ya pamoja yaliyofikiwa kati ya marais wawili, kudumisha mawasiliano ya ngazi ya juu na ngazi mbalimbali, kusukuma mbele mpango wa siku 100 wa ushirikiano wa kiuchumi, kupanua ushirikiano wa kihalisi katika sekta mbalimbali, na kuimarisha mawasiliano na uratibu katika masuala makubwa ya kimataifa na kikanda.

    Bw. Tillerson alisema Marekani inapenda kuimarisha uratibu na China ili kufanya maandalizi kwa duru ya kwanza ya mazungumzo ya usalama wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

    Pande mbili pia zimebadilishana maoni kuhusu masuala yanayofuatiliwa kwa pamoja ikiwemo hali ya peninsula ya Korea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako