• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yasema kutatua suala la nyuklia la peninsula ya Korea kwa nguvu za kijeshi kutasababisha msiba

    (GMT+08:00) 2017-05-20 18:40:46

    Waziri wa ulinzi wa Marekani Bw. James Mattis ameonya kuwa kutatua suala la nyuklia la peninsula ya Korea kwa nguvu za kijeshi kutasababisha msiba mkubwa.

    Amesema lengo la juhudi za Marekani ni kushirikiana na Umoja wa Mataifa, China, Japan na Korea Kusini ili kutafuta utatuzi wa suala hilo.

    Rais Donald Trump wa Marekani alipokutana na mjumbe maalum wa rais wa Korea Kusini Bw. Hong Seok-hyun tarehe 17 mjini Washington alisema Marekani inapenda kuwasiliana na Korea Kaskazini katika hali iliyo bora ili kutimiza amani ya huko.

    Tarehe 26 mwezi Aprili serikali ya Marekani ilisema itaiwekea Korea Kaskazini vikwazo vingi zaidi vya kiuchumi na kuishinikiza kwa njia ya kidiplomasia ili kutimiza hali ya kutokuwepo kwa silaha za nyuklia kwenye peninsula ya Korea. Marekani ina msimamo wazi kuhusu kutimiza lengo hilo kwa mazungumzo, lakini pia imejitayarisha kulinda usalama wa Marekani wa wenzi wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako