• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo ya duru ya sita kuhusu suala la Syria yafungwa bila mafanikio

    (GMT+08:00) 2017-05-20 19:10:02

    Mazungumzo ya duru ya sita kuhusu suala la Syria yaliyofanyika huko Geneva kwa uongozi wa Umoja wa Mataifa jana yamefungwa bila mafanikio yoyote. Mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Syria Bw. Staffan de Mistura amesema mazungumzo ya duru ijayo huenda yatafanyika mwezi Juni mwaka huu.

    Bw. de Mistura amesema pande mbalimbali zilijadili baadhi ya masuala kwenye mazungumzo hayo, lakini hazikufanya majadiliano kuhusu mada kuu nne za mazungumzo hayo zikiwemo kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, kurekebisha katiba, kufanya upya uchaguzi mkuu na kupambana na ugaidi. Ameyataka mazungumzo ya duru ijayo yazindue mapema majadiliano kuhusu mada hizo nne.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako