• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi kuu Tanzania Bara (VPL): Pazia lafungwa rasmi, Mbao FC yatia doa sherehe za ubingwa wa Yanga

    (GMT+08:00) 2017-05-22 08:47:06

    Pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara limefungwa jumamosi kwa vigogo, Simba na Yanga kumaliza na pointi sawa, 68 kila moja baada ya mechi 30.

    Hiyo inafuatia Simba kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Mwadui FC mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku Yanga wakichapwa 1-0 na Mbao FC uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

    Kwa matokeo hayo, Yanga imefanikiwa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu kwa wastani wake mzuri wa mabao, ingawa bado kuna tishio la Simba kwenda Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) mjini Zurich, Uswisi kudai pointi tatu za chee walizopokonywa baada ya kupewa kimakosa kufuatia kufungwa na Kagera Sugar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako