• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • La Liga: Real Madrid yaitwanga Malaga na kunyakua ubingwa

    (GMT+08:00) 2017-05-22 08:48:40

    Real Madrid wamekuwa mabingwa wapya wa La Liga baada ya kuichapa Malaga kwa mabao 2-0. Pamoja na ushindi wa Barcelona wa mabao 4-2 dhidi ya Eibar, haukuweza kuwazuia Madrid kubeba ubingwa kwa tofauti ya pointi 3.

    Bao la kwanza la Madrid lilifungwa na Cristiano Ronaldo na la pili lilifungwa na Karim Benzema. Madrid wamemaliza msimu wakiwa na alama 93 kwa michezo 38 wakifuatiwa na mahasimu wao Barcelona waliomaliza na alama 90.

    Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi amekuwa mfungaji bora wa ligi hiyo akimaliza na mabao 37, akifuatiwa na Luis Suarez, mwenye mabao 29, Cristiano Ronaldo akiwa katika nafasi ya tatu kwa magoli 25.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako