• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Kenya yasema China ni rafiki wa kuaminika kwenye ajenda ya mageuzi ya Kenya

    (GMT+08:00) 2017-05-22 09:20:08

    China imetajwa kuwa ni mdau wa kuaminika anayeisaidia Kenya kwenye utekekezaji wa ajenda yake ya mageuzi hasa kwenye ujenzi wa miundombinu.

    Akiongea na wana habari mjini Nairobi, Msemaji wa Ikulu ya Kenya Bw Manoah Esipisu amesema alama kubwa ya mageuzi hayo ni Reli kutoka Mombasa hadi Nairobi, ambayo imegharimu dola bilioni 3.6 za kimarekani, asilimia 90 ya hizo ukiwa ni mkopo kutoka benki ya Exim ya China.

    Bw Esipisu amesema Kenya inaamini kuwa miundombinu ni msingi wa maendeleo, na ndio maana alipoalikwa mjini Beijing na Rais Xi Jinping kuhudhuria mkutano kuhusu ujenzi wa miundombinu, alikubali kuhudhuria kwa furaha.

    Kenya inatarajiwa kuzindua reli ya Mombasa-Nairobi mwishoni mwa mwezi huu. China itatuma ujumbe wa maofisa waandamizi kuhudhuria uzinduzi wa reli hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako