• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa Tanzania na Uganda wasaini makubaliano ya ujenzi wa bomba la mafuta ghafi

    (GMT+08:00) 2017-05-22 09:24:06

    Rais John Magufuli wa Tanzania na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni wamesaini makubaliano ya kuanzisha mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima, Uganda hadi bandari ya Tanga Tanzania.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Tanzania, makubaliano hayo yamesainiwa mbele ya mawaziri na maofisa waandamizi kutoka taasisi mbalimbali zinazohusika na mradi huo. Pande mbili zilikuwa kwenye mazungumzo ya kuendelea na ujenzi huo baada ya kukubaliana bomba hilo lipitie Tanzania na sio Kenya kama ilivyopangwa awali. Marais hao wamewataka mawaziri wao wa nishati kusaini makubaliano kati ya serikali ijumaa hii, huko Kampala Uganda.

    Baada ya mradi huo kuanza kutekelezwa, bomba hilo lenye urefu wa kilomita 1,443 na litakalogharimu dola za kimarekani bilioni 3.55, litaweza kusafirisha lita laki mbili za mafuta kwa siku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako