• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China akutana na mwenzake wa Mali huko Bamako

    (GMT+08:00) 2017-05-22 09:47:29

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ambaye yuko ziarani nchini Mali, jana mjini Bamako alikutana na mwenzake wa Mali Bw. Abdoulaye Diop.

    Bw. Wang amesema, China na Mali ni marafiki wakubwa na uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeendelea kwa zaidi ya nusu ya karne. Amesema hivi sasa, Mali iko katika kipindi muhimu cha kihistoria, China inaunga mkono kithabiti juhudi za nchi hiyo katika kulinda mamlaka, usalama na umoja.

    Kwa upande wake Bw. Diop amesema, Mali inaishukuru China kwa misaada inayoipatia tangu ijipatie uhuru, na inapenda kuimarisha ushirikiano na China kupitia utekelezaji wa makubaliano ya Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, FOCAC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako