• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Donald Trump akutana na viongozi wa nchi za ghuba

    (GMT+08:00) 2017-05-22 10:08:31
    Rais Donald Trump wa Marekani anayefanya ziara nchini Saudi Arabia jana alikutana na viongozi wa nchi za Kamati ya Ushirikiano ya nchi za ghuba, na kujadili masuala kuhusu matishio ya kiusalama yanayoikabili kanda hiyo, kujenga mfumo wa ulinzi na kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Marekani na nchi za ghuba.

    Kabla ya mkutano huo, Marekani na kamati hiyo zilisaini makubaliano ya kuanzisha Kituo cha kupambana na utakatishaji wa fedha na ufadhili wa ugaidi.

    Rais Trump aliwasili nchini Saudi Arabia tarehe 20 na kuanza ziara yake ya kwanza tangu aingie madarakani. Kwenye ziara hiyo, rais Trump pia alisaini makubaliano ya kuiuzia Saudi Arabia vifaa vya kijeshi vyenye thamani ya dola bilioni 110 za kimarekani. Wizara ya mambo ya ndani ya Marekani imeyataja kuwa hatua ya kulinda usalama wa kanda ya Ghuba na kuimarisha uwezo wao wa kupambana na ugaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako