• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yapenda kuzisaidia nchi za Mashariki ya Kati kupambana na ugaidi

    (GMT+08:00) 2017-05-22 18:25:55

    Rais Donald Trump wa Marekani ambaye yuko ziarani nchini Saudi Arabia amesema nchi yake inapenda kuzisaidia nchi za Mashariki ya Kati kupambana na ugaidi, lakini pia ameeleza matumaini yake kwamba nchi hizo hazitaitegemea Marekani tu, bali zitashirikiana pamoja kupambana na ugaidi.

    Kwenye mkutano wa viongozi wa nchi zaidi ya 50 za kiarabu na kiislamu uliofanyika mjini Riyadh, rais Trump amesema ugaidi umeenea duniani kote, na Mashariki ya Kati ni kanda inayoathiriwa zaidi. Amezihimiza nchi za kanda hiyo zichukue hatua haraka kupambana na magaidi na watu wenye siasa kali, ili kuanzisha mustakabali wenye amani na utulivi kwa vizazi vijavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako