• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNHCR yaongeza misaada kwa wakimbizi wa Libya

    (GMT+08:00) 2017-05-22 18:25:34

    Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya wakimbizi Filippo Grandi amesema, Umoja huo utaongeza misaada ya kibindamu kwa Libya kwa kuwa nchi hiyo inahitaji misaada ya dharura ili kuboresha maisha ya wakimbizi.

    Akitembelea vituo vinavyopokea wakimbizi mjini Tripoli, Bw. Grandi amesema, hali ya Libya bado sio nzuri, na wakimbizi wengi wanaishi maisha magumu.

    Bw. Grandi pia amesema, licha ya kuongeza vituo vya kupokea wakimbizi, Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) litaendelea kushirikiana na mashirika mengine ya kimataifa kupanua eneo la uokoaji wa baharini, kuongeza sehemu za kuzuia wahamiaji haramu mipakani, na kutoa kipaumbele uokoaji wa maisha kwenye kazi ya uokoaji wa binadamu

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako