• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamworor na Mo Farah kufufua upya uhasama Ijumaa hii.

    (GMT+08:00) 2017-05-23 08:27:33

    Miamba wawili wa masafa marefu Geoffrey Kamworor na Muingereza Mo Farah watafufua uhasama wao katika mbio za mita 5000 Riadha za Diamond League zitakapoingia mkondo wa 3 mjini Eugene, Amerika Ijumaa hii.

    Katika orodha iliyotolewa na waandalizi wa mbio hizo, zaidi ya nusu ya wanariadha watakaoshiriki wanajivunia medali katika michezo ya Olimpiki au Riadha za Dunia.

    Farah ana dhahabu 4 za Olimpiki na 5 za dunia, zote zikiwa kutoka katika mbio za mita 5000 na 10000. Kamworor ndiye mwanariadha wa 2 mwenye idadi kubwa ya medali za dhahabu baada ya Farah.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako